Kuna jitihada nyingi za kumshirikisha mwanaume katika masuala ya afya ya uzazi zinayofanywa na serikali na mashirika binafsi ya kitaifa na kimataifa ikiwemo kupanga mikakati na sera zitakazoshawishi na kuvutia wanaume kufika katika hospitali na vituo vya afya ili kupata huduma za afya ya uzazi au kusindikiza wenza wao katika kliniki za awali na baada ya ujauzito. Moja kati ya mikakati kuhusu suala la kumshirikisha mwanaume katika afya ya uzazi ni kuanzishwa kwa huduma rafiki kwa wanaume wanaofika katika hospitali na vituo vya afya, mkakati unaotekelezwa na kusimamiwa na shirika la kimarekani la Engenderhealth chini ya mradi wa CHAMPION. Shirika hili limeweza kusaidia hospitali mbalimbali nchini Tanzania kutekeleza mkakati huu wa kumshirikisha mwanaume katika afya ya uzazi. Huduma hizi ni pamoja na kutoa kipaumbele cha huduma kwa wenzi waliohudhuria pamoja na motisha nyingine zinazobuniwa katika eneo husika. READ MORE