Madai ya Imani ya Biblia na mapokeo vyaathiri afya kwa wanawake:

KISA KUTOKA WILAYANI BUKOMBE

A.P. (44) ni mkazi wa kijiji cha Nampalahala, kata ya Busonzo katika wilaya ya Bukombe. Akiwa katika maeneo ya vijijini, mama huyu ameolewa na Mchungaji wa Kipentekoste aitwaye F.J. (50). A.P. anaishi umbali wa kilometa 82 kutokea makao makuu ya wilaya ya Bukombe, kiasi cha mwendo wa zaidi ya saa mbili kwa gari. Kituo cha afya cha karibu kiko Uyovu, umbali wa kilometa 20 kutoka mahali anapoishi Bi. A.P. Bi. A.P. ni mfano wa mamia ya maelfu ya wanawake wa Tanzania waishio vijijini ambao ndio wanaoongeza kasi ya uzazi nchini. Wakati Utafiti wa Afya na Idadi ya Watu wa mwaka 2010 ukionyesha kwamba wastani wa idadi ya watoto kwa wanawake wa vijijini wasio na elimu ni 7, kisa hiki kinaonyesha kiwango kisicho cha kawaida cha mwanamke mwenye ujauzito wa 14 na watoto 13 akisukumwa na madai ya kufuata mafundisho ya Biblia. Bi. A.P. hajawahi kutafuta huduma za uzazi wa mpango na anajitahidi kuwa mwaminifu kwa mumewe ambaye anataka aendelee kuzaa. Katika watoto 13 aliowazaa mama huyu, ni mmoja tu ambaye alijifungulia hospitalini na watoto hao wanapishana kwa miaka miwili miwili na mmoja mmoja. Mtoto wa kwanza (Paschael) ana umri wa miaka 25, mdogo zaidi (Sifa) ana umri wa miaka mitatu akifuatwa na ujauzito wa majuma 28. Kati ya watoto watano wa kwanza, ni mmoja tu ambaye amemaliza elimu ya msingi, wengine hawakumaliza. READ MORE